WAZIRI WA ULINZI WA MALI AUAWA

Date:

Share post:

BAMAKO, Mali

WAZIRI wa Ulinzi wa Mali, Sadio Camara, ameuawa katika shambulizi la kujitoa muhanga lililotekelezwa nje ya nyumba yake mjini Bamako.

Vyanzo mbalimbali vya habari vimeeleza kuwa kifo cha Camara ni sehemu ya mashambulizi ya vikundi vya kigaidi vilivyoota mizizi nchini humo.

Televisheni ya Taifa ya Mali imethibitisha kifo chake, ikieleza kuwa kilisababishwa na majeraha makubwa aliyopata katika shambulizi hilo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kiongozi wa jeshi anayeiongoza nchi hiyo, Jenerali Assimi Goita, amefichwa baada ya nyumba yake kuzingirwa na waasi.

Katika hatua nyingine, vikosi vya jeshi la Urusi vilivyopo Mali kwa ajili ya kulinda usalama, vimeripotiwa kuondoka mjini Kidal baada ya kuzidiwa na waasi wa Azawad Liberation Front (FLA).

Kwa miaka mingi, Mali imekuwa ikiandamwa na jinamizi la hali mbaya ya usalama inayotokana na utitiri wa vikundi vya kigaidi vinavyohusishwa na al-Qaeda na IS.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MEGAN AACHANA NA MPENZI WAKE KISA ‘KUCHEPUKA’

LOS ANGELES, Marekani BIBIYE mwenye jina kubwa katika soko la muziki wa Hip hop nchini Marekani, Megan thee stallion,...

SERIKALI YAWEKA WAZI MKAKATI WA KUIFANYA SEKTA YA MADINI KUWA MHIMILI WA UCHUMI

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 27, 2026,...

KINDA AJAX AZIGONGANISHA ARSENAL, CHELSEA

LONDON, Uingereza KLABU za Arsenal na Chelsea zimeingia kwenye vita ya kuiwania saini ya staa wa Ajax ya Uholanzi,...

MABORESHO YA UWANJA WA BENJAMINI MKAPA YAANZA RASMI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson...