MADRID, Hispania
KLABU ya Atletico Madrid iko kwenye harakati za kumsajili beki wa kulia wa Liverpool na timu ya taifa ya Scotland, Andy Robertson.
Atletico walijaribu bila mafanikio kumchukua Robertson wakati wa dirisha kubwa la usajili wa kiangazi, 2025.
Hata hivyo, kocha wa Atletico, Diego Simeone, amewaambia mabosi wa klabu hiyo kuwa bado anamuhitaji nyota huyo mwenye umri wa miaka 32.
Robertson ameshathibitisha kuwa huu ni msimu wake wa mwisho Anfield baada ya miaka tisa ya utumishi wake.
Uamuzi huo wa kuondoka umetokana na kupoteza nafasi ya kuingia kikosi cha kwanza chini ya kocha Arne Slot.






