Klabu ya Kaizer Chiefs imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu mpya baada ya kukamilisha usajili wa golikipa Renaldo Leaner, ambaye anatarajiwa kuongeza ushindani na uimara katika idara ya makipa.

Leaner, mwenye umri wa miaka 28 na mzaliwa wa Cape Town, anajiunga na Kaizer Chiefs akiwa na uzoefu wa kucheza katika kiwango cha juu.

Kiwango alichokionyesha msimu uliopita kilimuwezesha kuitwa mara kadhaa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana.

Uongozi wa Kaizer Chiefs umeeleza kuwa usajili wa Leaner ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha kikosi kuelekea msimu mpya, huku ukilenga kuongeza ushindani katika mashindano mbalimbali.

Mashabiki wa Kaizer Chiefs wamepokea kwa matumaini makubwa ujio wa golikipa huyo, wakiamini ataongeza ubora na utulivu kuanzia langoni na kuisaidia timu kufikia malengo yake.

Klabu hiyo pia imemkaribisha rasmi Leaner katika familia ya Khosi Nation, ikimtakia mafanikio makubwa akiwa na jezi ya Amakhosi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here