Klabu ya Atlético Madrid imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo mshambuliaji Kang-in Lee kutoka Paris Saint-Germain (PSG) katika dirisha la usajili.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, dili hilo lina thamani ya takribani euro milioni 40, ikiwa ni pamoja na bonasi zinazohusiana na makubaliano hayo.

Mchezaji huyo raia wa Korea Kusini anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano baada ya pande zote mbili kukubaliana masharti binafsi.

Kukamilika kwa usajili wa Kang-in Lee kunatajwa kuwa sehemu ya mpango wa Atlético Madrid wa kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Baada ya hatua hiyo, klabu hiyo inaelekeza nguvu zake katika kumsajili kiungo Morten Hjulmand, ambaye ametajwa kuwa ndiye lengo lao kuu linalofuata kwenye soko la usajili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here