Nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo, ameongoza tukio la kugusa hisia baada ya Portugal kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Croatia na kufuzu hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia.
Baada ya filimbi ya mwisho, Ronaldo alivaa jezi namba 21 aliyokuwa akiitumia marehemu Diogo Jota, kisha waliinua juu jezi hiyo akiwa pamoja na wachezaji wenzake huku akielekeza mkono angani kama ishara ya kumuenzi Jota na kaka yake, André Silva, waliofariki katika ajali ya gari mwaka mmoja uliopita.
Mbali na kuongoza heshima hiyo, Ronaldo aliifungia Portugal bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penalti kabla ya Gonçalo Ramos kufunga bao la ushindi katika dakika za nyongeza na kuipeleka Portugal hatua ya 16 bora, ambako itakutana na Hispania.
Tukio hilo la kumkumbuka Jota limegusa mioyo ya mashabiki wengi wa soka duniani.







