Beki kijana Kassoum Ouattara ameanza rasmi ukurasa mpya wa maisha yake ya soka baada ya kujiunga na Beşiktaş J.K. akitokea AS Monaco FC.
Ouattara anaondoka Monaco baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu mitatu, ambapo alicheza jumla ya mechi 57 katika mashindano mbalimbali na kutoa mchango muhimu ndani ya kikosi.
Katika kipindi hicho, pia alipata nafasi ya kucheza mechi tisa za Ligi ya Mabingwa Ulaya, hatua iliyomjengea uzoefu mkubwa wa soka la kiwango cha juu barani Ulaya.
Uhamisho wake kwenda Beşiktaş unatajwa kuwa hatua muhimu katika maendeleo ya taaluma yake, huku akitarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Wakala wake, Premier’Art, umeeleza kufurahishwa na kukamilika kwa uhamisho huo na kumtakia Ouattara kila la heri katika changamoto yake mpya akiwa na Beşiktaş JK.







