Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando (BMC), kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Sweden na Afrika Kusini, imefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa kurekebisha sura kwa wagonjwa sita.

Upasuaji huo umefanyika kupitia kambi maalumu ya siku tano iliyolenga kuwapatia wagonjwa huduma za kibingwa nchini, huku ukiwapunguzia gharama kubwa ambazo wangetumia kusafiri nje ya nchi kutafuta matibabu hayo.

Daktari Bingwa wa Upasuaji katika Hospitali ya Bugando, Dkt. Biswalo Yango, amesema mafanikio hayo ni sehemu ya dhamira ya BMC ya kushirikiana na kubadilishana uzoefu na madaktari bingwa wa kimataifa ili kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Baadhi ya wazazi wa watoto waliofanyiwa upasuaji huo wameishukuru hospitali hiyo, wakisema huduma hiyo imerejesha matumaini na kuboresha maisha ya watoto wao.

Huduma hiyo ya upasuaji wa kibingwa imetolewa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa afya waliofadhili gharama za matibabu, hatua iliyowawezesha wagonjwa kupata huduma hizo nchini bila kulazimika kusafiri nje ya nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here