Mwanamke Mmoja anayetambulika kwa jina la Neema Meleji (65) amefariki dunia papo hapo baada ya kukanyagwa na basi la kampuni ya HC katika stendi ya Dar Express jijini Arusha, alipokuwa akisubiri kupanda gari kuelekea Hospitali ya KCMC kwa ajili ya matibabu ya Afya yake.

Kwa mujibu wa mashuhuda waajali hiyo wamesema, ajali hiyo ilitokea wakati basi hilo lilipokuwa likirudishwa nyuma bila tahadhari, na kusababisha tairi za nyuma kumkanyaga mtu huyo katika eneo la kichwa, jambo lililosababisha kifo chake papo hapo .

Hatahivyo Askari wa Usalama Barabarani walifika eneo la tukio na kuuondoa mwili wa marehemu, ambapo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa ajili ya uchunguzi na taratibu nyingine za kisheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here