‎Vita kati ya Ukraine na Urusi vimechukua sura mpya baada ya Ukraine kutekeleza shambulizi kubwa la droni usiku kucha, likilenga maeneo muhimu ndani ya Urusi, yakiwemo mji wa St. Petersburg na mkoa wa Leningrad.

‎Kwa mujibu wa mamlaka za Urusi, mashambulizi hayo yaligonga kituo cha kuhifadhi mafuta pamoja na bandari ya kimkakati ya Vysotsk, huku vikosi vya ulinzi wa anga vikidai kufanikiwa kudungua makumi ya droni kabla ya kufika malengo yake.

‎Ingawa hakuna vifo vilivyoripotiwa, mashambulizi hayo yamezua taharuki kubwa kwa kuwa yalilenga miundombinu muhimu ya nishati na usafirishaji, hatua inayotafsiriwa kama pigo kwa mfumo wa usambazaji wa mafuta na shughuli za kijeshi za Urusi.

‎Shambulizi hili linaonyesha kuwa Ukraine inaendelea kupanua uwezo wake wa kushambulia maeneo ya mbali ndani ya Urusi, jambo linaloongeza presha mpya katika vita vinavyoendelea kati ya mataifa hayo mawili.

Imeandaliwa na Mariam Milondomo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here