Friday, 21 August 2026

MAMBA AVISHWA GAUNI LA HARUSI, AOLEWA NA MEYA

Meya wa mji wa San Pedro Huamelula, ulioko jimbo la Oaxaca nchini Mexico, amefunga ndoa ya kimila na mamba jike aina ya caiman katika sherehe ya jadi inayofanyika kila mwaka na kuvutia maelfu ya wakazi pamoja na wageni. Katika sherehe hiyo, mamba huyo huvalishwa gauni la harusi na kuzungushwa mitaani kabla ya kufikishwa kwenye hafla […]
Image ref 127171634. Copyright Shutterstock No reproduction without permission. See www.shutterstock.com/license for more information.

Meya wa mji wa San Pedro Huamelula, ulioko jimbo la Oaxaca nchini Mexico, amefunga ndoa ya kimila na mamba jike aina ya caiman katika sherehe ya jadi inayofanyika kila mwaka na kuvutia maelfu ya wakazi pamoja na wageni.

Katika sherehe hiyo, mamba huyo huvalishwa gauni la harusi na kuzungushwa mitaani kabla ya kufikishwa kwenye hafla rasmi ya ndoa, ambapo meya huwakilisha mfalme wa jamii ya Chontal huku mamba huyo akiwakilisha binti mfalme wa jamii ya Huave.

Kwa mujibu wa viongozi wa eneo hilo, mila hiyo imekuwepo kwa zaidi ya miaka 230 na inaashiria amani, umoja na ushirikiano kati ya jamii hizo mbili za asili. Pia huaminika kuleta mvua, mavuno mazuri, uvuvi wenye mafanikio na ustawi kwa jamii.

Ingawa hafla hiyo hufanana na ndoa halisi, ni sherehe ya kiutamaduni na ya kiishara inayolenga kuhifadhi urithi wa jamii za asili za Mexico na kuenzi uhusiano wao na mazingira.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *