Wednesday, 14 October 2026

RAIS TRUMP AFUNGUKA BAADA YA KUNUSURIKA KUUAWA

WASHINGTON DC, Marekani RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema hakuwa na hofu wakati wa shambulizi la risasi katika hafla ya waandishi wa habari wa Ikulu aliyohudhuria mjini Washington DC. Mwanaume mwenye umri wa miaka 31 aliyefahamika kwa jina la Cole Tomas Allen, ndiye aliyefyatua risasi jirani na eneo la ulinzi wa Rais Trump. Baada ya […]

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema hakuwa na hofu wakati wa shambulizi la risasi katika hafla ya waandishi wa habari wa Ikulu aliyohudhuria mjini Washington DC.

Mwanaume mwenye umri wa miaka 31 aliyefahamika kwa jina la Cole Tomas Allen, ndiye aliyefyatua risasi jirani na eneo la ulinzi wa Rais Trump.

Baada ya kusikika kwa milio ya risasi, walinzi walilazimika kumkimbiza na kumficha Rais Trump kwenye chumba maalumu.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Todd Blanche, amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa alilenga kuwadhuru viongozi wa utawala wa Rais Trump.

Akihojiwa baada ya tukio hilo, Rais Trump amesema: “Sikuogopa. Nayaelewa maisha. Tunaishi kwenye dunia yenye wendawazimu mwingi.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *