LOS ANGELES, Marekani
BIBIYE mwenye jina kubwa katika soko la muziki wa Hip hop nchini Marekani, Megan thee stallion, ametangaza kuachana na mpenzi wake, Klay Alexander Thompson.
Megan ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kutangaza taarifa hiyo, pia akisema chanzo ni mshikaji huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine.
Alexander Thompson ni mmoja ya mastaa wa Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA) akiwa na klabu ya Dallas Mavericks.
Katika hatua nyingine, Megan ambaye pia ni mwigizaji wa filamu amesema kwa sasa anahitaji kuwa ‘singo’ ili kuilinda afya yake ya akili.
Kwa upande wake, Alexander Thompson amedai kuwa mrembo huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza ‘kuchepuka’ na ndipo alipoamua kulipiza kisasi.
“Alikuwa wa kwanza kunisaliti, nikalipiza kisasi. Nimeumia kwa sababu nilitumia zaidi ya Dola milioni nne kwa ajili yake. Sitorudia,” amesema.






