Tuesday, 13 October 2026

BAYEN WAGOMA KUMBAKIZA JACKSON

MUNICH, Ujerumani BAYERN Munich wamethibitisha kuwa hawatomsajili moja kwa moja mshambuliaji wanayemtumia kwa mkopo kutoka Chelsea, Nicolas Jackson. Jackson alisajiliwa kwa mkopo mwaka jana na mkataba wake ulikuwa na kipengele kinachoiruhusu Bayern kumsajili kwa Pauni milioni 56.2. Nyota huyo amekuwa na mchango mkubwa kwa Bayern akishirikiana na Harry Kane, ambapo ameshafunga mabao matano na ‘asisti’ […]

MUNICH, Ujerumani

BAYERN Munich wamethibitisha kuwa hawatomsajili moja kwa moja mshambuliaji wanayemtumia kwa mkopo kutoka Chelsea, Nicolas Jackson.

Jackson alisajiliwa kwa mkopo mwaka jana na mkataba wake ulikuwa na kipengele kinachoiruhusu Bayern kumsajili kwa Pauni milioni 56.2.

Nyota huyo amekuwa na mchango mkubwa kwa Bayern akishirikiana na Harry Kane, ambapo ameshafunga mabao matano na ‘asisti’ mbili katika mechi saba zilizopita.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Michezo wa Bayern, Max Eberl, amefichua kuwa Jackson atarejea Chelsea mwishoni mwa msimu huu.

“Hatutotumia kipengele cha kumbakiza Nicolas Jackson,” amesema Eberl katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha ZDF.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *