MABORESHO YA UWANJA WA BENJAMINI MKAPA YAANZA RASMI

Date:

Share post:

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ametangaza kuanza kwa maboresho makubwa katika Uwanja wa Benjamin uliopo jijini Dar es Salaam.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Msigwa amesema kuwa marekebisho hayo yanahusisha sehemu ya kuchezea (Pitch), ambayo inatarajiwa kuwa ya kisasa ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo.

Amesema lengo ni kuwa na pitch yenye viwango vya juu vya Kimataifa, sambamba na kuboresha maeneo mengine ya uwanja ikiwemo lounges, vyumba vya kubadilishia nguo (changing rooms), ubao wa matokeo (Scoreboard) pamoja na mwonekano wa jumla (Branding).

Aidha, ameomba radhi kwa mashabiki wa soka kwa kutoweza kuutumia uwanja huo katika dabi ya Kariakoo iliyopangwa kufanyika Mei 3, 2026, akiahidi kuwa baada ya maboresho kukamilika, uwanja huo utakuwa katika hali bora zaidi kwa matumizi ya muda mrefu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MEGAN AACHANA NA MPENZI WAKE KISA ‘KUCHEPUKA’

LOS ANGELES, Marekani BIBIYE mwenye jina kubwa katika soko la muziki wa Hip hop nchini Marekani, Megan thee stallion,...

SERIKALI YAWEKA WAZI MKAKATI WA KUIFANYA SEKTA YA MADINI KUWA MHIMILI WA UCHUMI

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 27, 2026,...

KINDA AJAX AZIGONGANISHA ARSENAL, CHELSEA

LONDON, Uingereza KLABU za Arsenal na Chelsea zimeingia kwenye vita ya kuiwania saini ya staa wa Ajax ya Uholanzi,...

ANTONIO CONTE ATAJWA KURUDI CHELSEA

LONDON, Uingereza HUENDA kocha raia wa Italia, Antonio Conte, akarejea kuliongoza benchi la ufundi la Chelsea lililoachwa wazi na...