Tuesday, 13 October 2026

ANTONIO CONTE ATAJWA KURUDI CHELSEA

LONDON, Uingereza HUENDA kocha raia wa Italia, Antonio Conte, akarejea kuliongoza benchi la ufundi la Chelsea lililoachwa wazi na Liam Rosenior. Conte anainoa Napoli kwa sasa lakini zipo taarifa kuwa ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu. Mkataba wake na vigogo hao wa Serie A utafikia ukomo mwishoni mwa msimu ujao (2027-28). Alikuwa na mafanikio […]

LONDON, Uingereza

HUENDA kocha raia wa Italia, Antonio Conte, akarejea kuliongoza benchi la ufundi la Chelsea lililoachwa wazi na Liam Rosenior.

Conte anainoa Napoli kwa sasa lakini zipo taarifa kuwa ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Mkataba wake na vigogo hao wa Serie A utafikia ukomo mwishoni mwa msimu ujao (2027-28).

Alikuwa na mafanikio makubwa msimu uliopita, ambapo aliipa Napoli taji la Ligi Kuu hiyo ya Italia.

Kwa siku za hivi karibuni, Conte amekuwa akihusishwa na kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Italia.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *