ILO: MAENEO YA KAZI HUSABABISHA VIFO 840,000 KILA MWAKA

Date:

Share post:

HIYO ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), ikieleza namna mazingira ya kazi yanavyoweza kuhatarisha afya na kusababisha kifo kwa mwajiriwa.

Iko hivi; kwa mujibu wa ILO, watu zaidi ya 840,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokanana na mazingira yao ya kazi.

Katika ripoti hiyo, ILO imesema mazingira yanayoweza kuharibu afya na hata kusababisha kifo cha mwajiriwa ni pamoja na kufanya kazi muda mrefu, kutokujua hatima yake, malipo kiduchu yasiyoendana na jitihada zake, na hata manyanyaso ya bosi wake.

Utafiti wa ILO umefafanua kuwa asilimia 35 ya waajiriwa duniani kote hufanya kazi kwa saa zaidi ya 48 kwa wiki.

Kama hiyo haitoshi, asilimia 23 wameshawahi kukumbana na msongo wa mawazo kutokana na manyanyaso kutoka kwa waajiri wao.

Kwa mujibu wa ILO, mazingira ya aina hiyo huathiri afya ya mwajiriwa, ikiwamo kumsababishia msongo wa mawazo unaoweza kuzalisha shinikizo la damu, magonjwa ya moy o, kiarusi, na hata kujiua.

“Hatari za kisaikolojia zimekuwa moja ya changamoto kubwa katika maeneo mengi ya kazi,” amesema Kiongozi wa Timu ya Mifumo ya Usalama wa Maeneo ya Kazi wa ILO, Manal Azzi.

“Kuna umuhimu mkubwa wa kuboresha saikolojia katika mazingira ya kazi, si tu kwa ajili ya kuwalinda waajiriwa, bali pia itaongeza uzalishaji, kuboresha utendaji wa taasisi na kuongeza uchumi.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MEGAN AACHANA NA MPENZI WAKE KISA ‘KUCHEPUKA’

LOS ANGELES, Marekani BIBIYE mwenye jina kubwa katika soko la muziki wa Hip hop nchini Marekani, Megan thee stallion,...

SERIKALI YAWEKA WAZI MKAKATI WA KUIFANYA SEKTA YA MADINI KUWA MHIMILI WA UCHUMI

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 27, 2026,...

KINDA AJAX AZIGONGANISHA ARSENAL, CHELSEA

LONDON, Uingereza KLABU za Arsenal na Chelsea zimeingia kwenye vita ya kuiwania saini ya staa wa Ajax ya Uholanzi,...

MABORESHO YA UWANJA WA BENJAMINI MKAPA YAANZA RASMI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson...