UPASUAJI WA KUKUZA MATITI WAPUNGUA

Date:

Share post:

KWA mara ya kwanza katika historia ya Uingereza, idadi ya wanawake wanaofanya upasuaji wa kupunguza ukubwa wa matiti imekuwa kubwa kuliko ya wanaoongeza.

Hilo limethibitishwa na utafiti wa Chama cha Wataalamu wa Upasuaji wa Kubadili Mwonekano nchini humo (BAAPS).

Katika ripoti yao, watafiti wa BAAPS wamebaini kuwa matukio ya kuongeza ukubwa wa matiti yalipungua kwa asilimia 8 mwaka 2025.

“Kwa mwaka 2025, ni matukio 4,761 pekee, sawa na upungufu wa asilimia 8, ukilinganisha na takwimu za mwaka 2024,” imeeleza ripoti ya BAAPS.

Akizungumza matokeo ya utafiti wao, Rais wa BAAPS, Nora Nugent, amesema: “Kwa mara ya kwanza, tumeshuhudia ongezeko kubwa la upasuaji wa kupunguza ukubwa wa matiti.

“Wagonjwa wengi (waliopunguza ukubwa wa matiti), wameeleza sababu kuwa ni kutaka uhuru zaidi wakiwa wanafanya mazoezi.

“Wengine wanasema ukubwa wa matiti unawafanya washindwe kuvaa baadhi ya nguo wanazozipenda.”

Aidha, watafiti wa Chama hicho wamegundua ongezeko la asilimia 27 la matukio ya upasuaji wa kurekebisha mwonekano wa uso.

Katika hatua nyingine ya utafiti, BAAPS wameeleza kuwa bado wanawake ndiyo wateja wakubwa wa upasuaji wa kubadili mwonekano, ikiwamo kuongeza au kupunguza ukubwa wa matiti na makalio.

“Katika matukio yote 25,217 ya mwaka 2025, asilimia 93.9 ni wanawake. Hata hivyo, idadi imepungua kwa asilimia 2, ukilinganisha na mwaka 2024,” imeeleza ripoti ya utafiti huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

MEGAN AACHANA NA MPENZI WAKE KISA ‘KUCHEPUKA’

LOS ANGELES, Marekani BIBIYE mwenye jina kubwa katika soko la muziki wa Hip hop nchini Marekani, Megan thee stallion,...

SERIKALI YAWEKA WAZI MKAKATI WA KUIFANYA SEKTA YA MADINI KUWA MHIMILI WA UCHUMI

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 27, 2026,...

KINDA AJAX AZIGONGANISHA ARSENAL, CHELSEA

LONDON, Uingereza KLABU za Arsenal na Chelsea zimeingia kwenye vita ya kuiwania saini ya staa wa Ajax ya Uholanzi,...

MABORESHO YA UWANJA WA BENJAMINI MKAPA YAANZA RASMI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson...