Tumaini Makene |
NA MWANDISHI WETU
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza masikitiko yake dhidi ya watu wanaokichafua katika mitandao ya kijamii.
Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Chadema, Tumaini Makene alisema watu wenye nia ovu na chama hicho wamekuwa wakisambaza ujumbe wa kupotosha katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwatisha au kuibua taharuki kwa wanachama, wafuasi na mashabiki wa chama.
Alisema barua iliyosambaa jana mitandaoni inayoonyesha kuandikwa na kusainiwa naye, Septemba 5, 2020 ni kielelezo cha matendo machafu kinachofanyiwa Chadema na watu wasiokitakia mema.
Freeman Mbowe |
“Barua ya uongo yenye ujinga kama hiyo wanaweza kuamini tu waliyoitengeneza kujifurahisha kwa mahitaji yao wenyewe kaka,” alisema Makene.
Barua hiyo yenye kichwa cha maneno ‘chama cha demokrasia na maendeleo, taarifa kwa viongozi wote wa kanda’ inaonyesha kusainiwa na Makene na inasomeka;
“Kichwa cha habari tajwa chahusika. Rejeeni kikao cha tarehe 25.08.2020 ambacho kilikuwa ni kikao kazi na tathimini ya hali ya fedha kuelekea uchaguzi mkuu 2020.
“Naomba kuwajulisheni rasmi kuwa tutawezesha kwa asilimia 25 tu na inayosalia tumieni mfumo wa harambee licha ya ugumu uliopo hasa ukizingatia wafadhili wote wa ndani kuhofu kutuchangia kwa sababu za kisiasa.
“Pia tuna taarifa kuwa yapo majimbo ambayo wagombea wetu wameishaingiwa na wasiwasi wa ushindi na tayari dhamira zao zinatupa mashaka. Hili halikubaliki na tayari tumeishawatumia timu ya kuchunguza ili kujitathimini kabla ya awamu ya kwanza ya kampeni kwa mujibu wa vikao vyao vya ndani. Lazima mapambano yaendelee.