MANCHESTER, Uingereza
KATIKA ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burnley, kiungo wa Manchester City, Bernardo Silva, ameweka rekodi ya kibabe Ligi Kuu ya England (EPL).
Man City ikiwa ugenini katika Uwanja wa Turf Moor, ilipata bao hilo kupitia kwa Erling Haaland, hivyo kuing’oa kileleni Arsenal baada ya kuizidi mabao ya kufunga.
Matokeo hayo yamewafanya vijana wa Pep Guardiola kushinda mechi tano mfululizo za mashindano mbalimbali walizocheza hivi karibuni.
Bernardo mwenye umri wa miaka 31, anakuwa mchezaji wa Man City aliyeshinda mechi nyingi za EPL (215) katika historia ya klabu hiyo ya jijini Manchester.
Kabla ya mchezo huo dhidi ya Burnley, rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na kiungo wa zamani wa timu hiyo, David Silva.
Kwa msimu huu, Bernardo amecheza mechi 46 za michuano mbalimbali, akidiwa na Nico O’Reilly (48) na Haaland (47) pekee.






