ISRAEL YASHUTUMIWA MAUAJI YA MWANDISHI LEBANON

Date:

Share post:

BEIRUT, Lebanon

LEBANON imeishutumu Israel ikiihusisha na kifo cha mwandishi wa habari aliyeuawa katika shambulizi la anga.

Amal Khalil aliuawa akiwa kwenye majukumu yake, ikielezwa kuwa ni mwandishi wa Gazeti la Al-Akhbar nchini Lebanon.

Katika shambulizi hilo la juzi Aprili 21, 2026, mwandishi mwingine, Zeinab Faraj, aliripotiwa kujeruhiwa.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Lebanon imesema kinachofanywa na Israel nchini kwake ni uhalifu wa kivita.

Kwa mujibu wa viongozi wa Israel, Khalil na Zeinab walilengwa katika shambulizi hilo lililoua watu wawili.

Hayo yanakuja wakati Israel na Lebanon kukaa kwenye meza ya mazungumzo leo Aprili 23, 2026 mjini Washington.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RAIS WA UTURUKI AIONYA ULAYA KUHUSU IRAN

ISTANBUL, Uturuki RAIS wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema vita kati ya Iran na Marekani vimeanza kulidhohofisha Bara la...

TRENI ZAGONGANA NA KUJERUHI ABIRIA 10 DENMARK

COPENHAGEN, DenmarkAJALI ya treni mbili za abiria zilizogongana imesababisha watu wanaotajwa kufikia 10 kujeruhiwa nchini Denmark. Kwa mujibu wa...

MABORESHO YA MKOA WA KATAVI KUWEKWA KWENYE GRIDI YA TAIFA YA UMEME YA KAMILIKA

Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Serikali imekamilisha kuunganisha Mkoa wa Katavi katika Gridi ya Taifa na hivyo...

WANANCHI PWANI KUNUFAIKA NA UJENZI BARABARA YA KIMANZICHANA – MSANGA

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewahakikishia wakazi wa Kimanzichana mkoani Pwani kuwa Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili...