WANANCHI PWANI KUNUFAIKA NA UJENZI BARABARA YA KIMANZICHANA – MSANGA

Date:

Share post:

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewahakikishia wakazi wa Kimanzichana mkoani Pwani kuwa Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati yenye lengo la kuinua uchumi na kuwahimiza wananchi kuunga mkono juhudi hizo ili kufanikisha maendeleo endelevu.

Akizungumza baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya kilometa 43.83 kutoka Kimanzichana kupitia Mkamba hadi Msanga, Ulega amesema kuwa Serikali tayari imeshatoa fedha zinazohitajika na kwamba maandalizi ya utekelezaji yako katika hatua za mwisho.

Waziri huyo aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza hivi karibuni mara baada ya msimu wa masika kumalizika. Pia aliagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kusimamia kwa karibu mradi huo ili kuhakikisha unatekelezwa kwa ubora na kwa wakati.

Aidha, Ulega alielekeza Meneja wa mradi kutoa kipaumbele cha ajira za muda kwa wakazi wa eneo hilo, akisema hatua hiyo itasaidia kuongeza kipato cha wananchi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kwa upande wao, wakazi wa Kimanzichana walioshiriki mkutano wa hadhara walieleza shukrani zao kwa serikali kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha za mradi huo. Wamesema kukamilika kwa barabara hiyo kutarahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, hasa mazao ya kilimo na biashara ndogondogo, hivyo kuboresha maisha yao kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RAIS WA UTURUKI AIONYA ULAYA KUHUSU IRAN

ISTANBUL, Uturuki RAIS wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema vita kati ya Iran na Marekani vimeanza kulidhohofisha Bara la...

ISRAEL YASHUTUMIWA MAUAJI YA MWANDISHI LEBANON

BEIRUT, Lebanon LEBANON imeishutumu Israel ikiihusisha na kifo cha mwandishi wa habari aliyeuawa katika shambulizi la anga. Amal Khalil aliuawa...

TRENI ZAGONGANA NA KUJERUHI ABIRIA 10 DENMARK

COPENHAGEN, DenmarkAJALI ya treni mbili za abiria zilizogongana imesababisha watu wanaotajwa kufikia 10 kujeruhiwa nchini Denmark. Kwa mujibu wa...

MABORESHO YA MKOA WA KATAVI KUWEKWA KWENYE GRIDI YA TAIFA YA UMEME YA KAMILIKA

Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Serikali imekamilisha kuunganisha Mkoa wa Katavi katika Gridi ya Taifa na hivyo...