Tuesday, 13 October 2026

TRENI ZAGONGANA NA KUJERUHI ABIRIA 10 DENMARK

COPENHAGEN, DenmarkAJALI ya treni mbili za abiria zilizogongana imesababisha watu wanaotajwa kufikia 10 kujeruhiwa nchini Denmark. Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya ndani na nje, ajali hiyo ilitokea jana Aprili 22, 2026 mjini Hillerod, Kaskazini mwa Mji Mkuu wa Copenhagen. “Kulikuwa na majeruhi miongoni mwa abiria waliokuwa kwenye treni hiyo,” imeeleza […]

COPENHAGEN, Denmark
AJALI ya treni mbili za abiria zilizogongana imesababisha watu wanaotajwa kufikia 10 kujeruhiwa nchini Denmark.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya ndani na nje, ajali hiyo ilitokea jana Aprili 22, 2026 mjini Hillerod, Kaskazini mwa Mji Mkuu wa Copenhagen.

“Kulikuwa na majeruhi miongoni mwa abiria waliokuwa kwenye treni hiyo,” imeeleza taarifa ya Idara ya Zimamoto ya Copenhagen.

Katika hatua nyingine, mamlaka zimeeleza kuwa bado zinaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *