CHOBWEDO AKABIDHIWA KIATU CHA DOLA 400 NA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

Date:

Share post:

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, amekutana na kuzungumza, pamoja na kumpatia zawadi ya viatu pamoja na vitu mbalimbali mchezaji nyota na winga wa TRA United, Ramadhan Salum maarufu kama “Chobwedo”, akimsifu kwa kiwango bora anachokionesha katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Makalla, ambaye pia ni mlezi wa timu hiyo yenye makazi yake mkoani Arusha, amesema Chobwedo ameonesha kiwango kizuri katika mechi za TRA dhidi ya Yanga pamoja na mechi mbili za Simba dhidi ya TRA zilizochezwa jijini Dar es Salaam na Arusha, na mechi dhidi ya Pamba Jiji.

Aidha, amemtaka mchezaji huyo kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, akisisitiza asikubali ukosoaji wa watumiaji wa mitandao hiyo kumvunja moyo.

“Mimi nimecheza mpira katika kiwango kikubwa lakini pia nimefundisha, kwa hiyo nikikupa sifa nakupa sifa za ukweli. Wewe Chobwedo ni mali. Nimefuatilia mechi zenu nikiwa nje ya nchi, huko Uturuki, nikasema nikuletee zawadi ya ‘bei mbaya’, kiatu chapa ya Nike chenye thamani ya dola 400 za Marekani, zaidi ya shilingi milioni moja za Kitanzania. Nakutakia kila la heri, nenda kapambane,” amesema Makalla.

Kwa upande wake, nyota huyo wa TRA United aliyetajwa kuwa mchezaji bora katika mechi kadhaa za hivi karibuni, amemshukuru RC Makalla kwa malezi yake kwa timu hiyo tangu ilipohamia mkoani Arusha, pamoja na zawadi aliyompatia.

Ramadhan Salum ameahidi kuendelea kupambana ili kutimiza malengo ya timu yake ya TRA United.

Katika msimu huu, Chobwedo amekuwa gumzo kutokana na kiwango chake cha juu, akishinda tuzo ya mchezaji bora wa mchezo (Man of the Match) mara kadhaa dhidi ya Tanzania Prisons, Yanga na Singida Big Stars, hali iliyochochea tetesi kuwa baadhi ya vigogo wa soka nchini wanamuwinda kwa ajili ya msimu ujao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RAIS WA UTURUKI AIONYA ULAYA KUHUSU IRAN

ISTANBUL, Uturuki RAIS wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema vita kati ya Iran na Marekani vimeanza kulidhohofisha Bara la...

ISRAEL YASHUTUMIWA MAUAJI YA MWANDISHI LEBANON

BEIRUT, Lebanon LEBANON imeishutumu Israel ikiihusisha na kifo cha mwandishi wa habari aliyeuawa katika shambulizi la anga. Amal Khalil aliuawa...

TRENI ZAGONGANA NA KUJERUHI ABIRIA 10 DENMARK

COPENHAGEN, DenmarkAJALI ya treni mbili za abiria zilizogongana imesababisha watu wanaotajwa kufikia 10 kujeruhiwa nchini Denmark. Kwa mujibu wa...

MABORESHO YA MKOA WA KATAVI KUWEKWA KWENYE GRIDI YA TAIFA YA UMEME YA KAMILIKA

Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Serikali imekamilisha kuunganisha Mkoa wa Katavi katika Gridi ya Taifa na hivyo...