RAIS WA UTURUKI AIONYA ULAYA KUHUSU IRAN

Date:

Share post:

ISTANBUL, Uturuki

RAIS wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema vita kati ya Iran na Marekani vimeanza kulidhohofisha Bara la Ulaya.

Tayyip Erdogan ameyasema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier.

Taarifa ya Ikulu ya Uturuki imeeleza kuwa viongozi hao walifanya mazungumzo hayo juzi Aprili 21, 2026.

Mbali ya kuzungumzia namna ya kuimarisha uhusiano wa Uturuki na Ujerumani, pia waligusia mgogoro huo wa Mashariki ya Kati.

“Rais Erdoaan alisema kuwa vita hivyo vimeanza kuidhohofisha Ulaya na kama hatua hazitochuliwa, basi hali itakuwa mbaya zaidi,” ilieleza taarifa hiyo.

Bado viongozi wa Marekani na Iran hazijafikia makubaliano ya kukaa tena mezani kusaka suluhu tangu waliposhindwa kufikia mwafaka katika mazungumzo ya awali mjini Islamabad.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

ISRAEL YASHUTUMIWA MAUAJI YA MWANDISHI LEBANON

BEIRUT, Lebanon LEBANON imeishutumu Israel ikiihusisha na kifo cha mwandishi wa habari aliyeuawa katika shambulizi la anga. Amal Khalil aliuawa...

TRENI ZAGONGANA NA KUJERUHI ABIRIA 10 DENMARK

COPENHAGEN, DenmarkAJALI ya treni mbili za abiria zilizogongana imesababisha watu wanaotajwa kufikia 10 kujeruhiwa nchini Denmark. Kwa mujibu wa...

MABORESHO YA MKOA WA KATAVI KUWEKWA KWENYE GRIDI YA TAIFA YA UMEME YA KAMILIKA

Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Serikali imekamilisha kuunganisha Mkoa wa Katavi katika Gridi ya Taifa na hivyo...

WANANCHI PWANI KUNUFAIKA NA UJENZI BARABARA YA KIMANZICHANA – MSANGA

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewahakikishia wakazi wa Kimanzichana mkoani Pwani kuwa Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili...