Tuesday, 13 October 2026

MABORESHO YA MKOA WA KATAVI KUWEKWA KWENYE GRIDI YA TAIFA YA UMEME YA KAMILIKA

Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Serikali imekamilisha kuunganisha Mkoa wa Katavi katika Gridi ya Taifa na hivyo kuimarisha upatikanaji wa umeme katika mkoa huo pamoja na kulipunguzia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) gharama za uzalishaji wa umeme kwa kutumia mafuta katika mkoa huo, ambapo jumla ya shilingi bilioni 68.4 zimeokolewa. Aidha, Ndejembi amesema kwa […]

Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Serikali imekamilisha kuunganisha Mkoa wa Katavi katika Gridi ya Taifa na hivyo kuimarisha upatikanaji wa umeme katika mkoa huo pamoja na kulipunguzia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) gharama za uzalishaji wa umeme kwa kutumia mafuta katika mkoa huo, ambapo jumla ya shilingi bilioni 68.4 zimeokolewa.

Aidha, Ndejembi amesema kwa upande wa usafirishaji wa umeme, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma, yenye urefu wa kilomita 345 umefikia asilimia 74.13.

Ndejembi amesema hayo leo Aprili 22, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *