CIUDAD DE LA PAZ, Guinea
AKIWA ziarani nchini Guinea ya Ikweta, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, amelaani vitendo vya rushwa, pia akihimiza usawa.
Guinea ya Ikweta imekuwa kituo chake cha mwisho katika ziara yake ya siku 11 kwa mataifa manne ya Afrika. Alishafika Algeria, Cameroon na Angola.
Pia, katika ibada yake iliyohudhuriwa pia na Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, Papa alihimiza umuhimu wa usawa na utawala bora.
Rais Mbasogo amekuwa madarakani tangu mwaka 1979, hivyo kwa sasa anashikilia rekodi ya kuwa ndiye kiongozi aliyehudumu muda mrefu zaidi duniani.
“Lazima uwepo uwanja mpana wa watu kuwa huru. Utu wa mtu unapaswa kuwa kipaumbele kwa namna yoyote ile.”






