MABOSI WAMTAKA BRUNO KUBAKI UNITED

Date:

Share post:

MANCHESTER, Uingereza

UONGOZI wa klabu ya Manchester United uko tayari kufanya lolote ili kumbakiza kiungo wake raia wa Ureno, Bruno Fernandes.

Kwa wiki za hivi karibuni, zimekuwapo taarifa kuwa huu ni msimu wa mwisho kwa nahodha huyo kukipiga Old Trafford.

Klabu tajiri ya Saudi Arabia, Al-Nassr, inatajwa kutenga kitita cha Pauni milioni 80 kukamilisha usajili wa nyota huyo.

Alikaribia kuondoka wakati wa usajili wa dirisha dogo la Januari, 2026 lakini kocha wa wa wakati huo, Ruben Amorim, alimshawishi kubaki.

Ni wakati ambao Bruno katika moja ya mahojiano yake, alisema baadhi ya vigogo wa klabu hiyo hawataki kumuona akibaki.

Safari hii, viongozi wa Man United wamefanya mazungumzo na Bruno na kumwambia nia yao ni kumbakiza kikosini kwa gharama yoyote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

GUARDIOLA AMPONZA KOCHA WA BURNLEY

LONDON, Uingereza KOCHA wa Burnley, Scott Parker, amekalia kuti kavu baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Manchester...

BERNARDO AWEKA REKODI MPYA MAN CITY

MANCHESTER, Uingereza KATIKA ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burnley, kiungo wa Manchester City, Bernardo Silva, ameweka rekodi ya...

CESC FABREGAS KOCHA MPYA CHELSEA?

LONDON, Uingereza KLABU ya Chelsea inaangalia uwezekano wa kumkabidhi benchi la ufundi kiungo wao wa zamani raia wa Hispania,...

PAPA LEO AKEMEA RUSHWA AKIWA GUINEA

CIUDAD DE LA PAZ, Guinea AKIWA ziarani nchini Guinea ya Ikweta, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV,...