LONDON, Uingereza
KOCHA wa Burnley, Scott Parker, amekalia kuti kavu baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Manchester City, matokeo yaliyoishusha Daraja msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Man City, ambayo sasa iko kileleni mwa msimamo wa EPL kwa tofauti ya mabao, ilipata ushindi huo kwa bao la mapema (dk. 5) la Erling Haaland.
Msimu huu, mabosi wa Burnley walikomaa na Parker, licha ya timu hiyo kushinda mechi moja pekee kati ya 25 za Ligi za hivi karibuni.
Hata hivyo, ripoti zilizopo zinaeleza kuwa mabosi wa klabhu hiyo wanasaka kocha mpya wa kuiongoza timu yao huko Championship.
Akizungumzia hatima yake baada ya Burnley kushuka dareaja, kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 amesema: “Ni kawaida kwa kocha kupitia nyakati hizi. Hatukuwa na msimu mzuri.”






