CESC FABREGAS KOCHA MPYA CHELSEA?

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Chelsea inaangalia uwezekano wa kumkabidhi benchi la ufundi kiungo wao wa zamani raia wa Hispania, Cesc Fabregas.

Mabosi wa Chelsea wamemfuta kazi Liam Rosenior baada ya timu hiyo kupoteza mechi tano mfululizo za Ligi Kuu ya England (EPL).

Rosenior raia wa England, amekuwa kwenye benchi kwa wiki 15 pekee tangu alipoajiriwa kwa mkataba wa miaka sita na nusu.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 41, aliajiriwa katikati ya msimu huu ili kuziba pengo la Enzo Maresca aliyefukuzwa Januari, 2026.

Fabregas ni miongoni mwa makocha wanaofanya vizuri Ligi Kuu ya Italia (Serie A) akikinoa kikosi cha Como 1907.

Hata hivyo, winga wa zamani wa Chelsea, Florent Malouda, amesema klabu hiyo itakuwa imecheza kamari kumpa kazi Fabregas.

Malouda raia wa Ufaransa, amesema bado kiungo huyo wa zamani wa Arsenal hajaiva vya kutosha kukabidhiwa timu kubwa aina ya Chelsea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

GUARDIOLA AMPONZA KOCHA WA BURNLEY

LONDON, Uingereza KOCHA wa Burnley, Scott Parker, amekalia kuti kavu baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Manchester...

BERNARDO AWEKA REKODI MPYA MAN CITY

MANCHESTER, Uingereza KATIKA ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burnley, kiungo wa Manchester City, Bernardo Silva, ameweka rekodi ya...

MABOSI WAMTAKA BRUNO KUBAKI UNITED

MANCHESTER, Uingereza UONGOZI wa klabu ya Manchester United uko tayari kufanya lolote ili kumbakiza kiungo wake raia wa Ureno,...

PAPA LEO AKEMEA RUSHWA AKIWA GUINEA

CIUDAD DE LA PAZ, Guinea AKIWA ziarani nchini Guinea ya Ikweta, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV,...