ZITTO SIYO MPENZI WANGU

Date:

Share post:

Salma Said

 

NA MWANDISHI WETU

MWANAHARAKATI Salma Said amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikumuhusisha na uhusiano wa kimapenzi na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Akizungumza na TANZANIA PANORAMA Blog jana kuhusu taarifa za ndoa yake kuvunjika baada ya kufumaniwa na mumewe akiwa na Zitto, alisema haijavunjika na hana uhusiano naye wala hafahamiani naye.

Salma alisema taarifa zinazo muhusisha kimapenzi na Zitto aliziona mitandaoni tangu Ijumaa wiki iliyopita lakini alizipuuza kwa sababu anajua zina lenga kumziba mdomo ili asisimamie anayoyaamini katika shughuli zake za kiunaharaka.

Hata hivyo, Salma ambaye pia ni Mwandishi wa habari alihoji kama maswali anayoulizwa na TANZANIA PANAROMA Blog yanalenga kutumika kuandika habari na alipoelezwa lengo ni hilo aliomba habari hiyo isiandikwe.

“Wananichafua, Zitto siyo mpenzi wangu wala simjui. Sina chama mimi ni mwanaharakati. Wanataka tu kunifunga mdomo lakini siogopi wala sinyamazi.

“Yaani hata sijui kwanini hawa watu wa CCM  na serikali wananiogopa. Tatizo la Zanzibar ukisema ukweli wanakuita mpinzani. Lakini mimi nilishazoea kuzushiwa kama unakumbuka hata nikipotekwa wakati ule walizusha kuwa nilikuwa nimefichwa na bwana mahali.

“Hiyo kitu sisi tuliiona mitandaoni tangu Ijumaa na nilipoiona tu nilimrushia mume wangu, yeye yupo Dar, akaniuliza nani kaandika nikamwambia apuuze,” alisema Salma.

Zitto


Alipotafutwa Zitto simu yake ilionyesha inatumika muda wote na alipofatutwa Afisa Habari wa ACT Wazalendo, Arodia Peter alisema hana taarifa kuhusu hilo na kushauri atafutwe Zitto mwenyewe kulizungimzia na kutoa namba ya Zitto inayopatikana.

TANZANIA PANORAMA Blog lilimpigia tena Zitto  kwa namba iliyotolewa na Arodia ambayo pia ilionyesha inatumika muda wote na hata alipotumiwa ujumbe mfupi kwenye simu yake hakujibu.

Tangu mwishoni mwa wiki iliyopita kumekuwa taarifa zinazodai kuwa Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto amevunja ndoa ya Salma na kwamba mume wake amehamia jijini Dar es Salaam.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

ISRAEL, LEBANON ZAONGEZA WIKI TATU ZA KUSITISHA VITA

WASHINGTON DC, Marekani RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema Israel na Lebanon zimekubaliana kuongeza wiki tatu za kusitisha mapigano. Wakati...

RAIS RAMAPHOSA ‘AMTUMBUA’ MKUU WA POLISI

PRETORIA, Afrika Kusini RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ametengua uteuzi wa Mkuu wa Polisi nchini humo, Jenerali Fannie...

PAPA AKOSOA MATESO YA WAFUNGWA GUINEA

MALABO, Guinea ya Ikweta KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, ameeleza kutokuridhishwa na namna wafungwa wanavyoishi katika...

LEAO AINGIA RADA ZA UNITED, LIVERPOOL

MILAN, Italia MANCHESTER United na Liverpool zimeingia kwenye ushindani mkali wa kuiwania saini ya winga wa AC Milan, Rafael...