LONDON, Uingereza
KLABU ya Manchester City inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez, wakati wa usajili wa kiangazi.
Kwa wiki za hivi karibuni, Muargentina huyo amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Stamford Bridge.
Man City nayo inamtolea macho Enzo, licha ya kuwapo kwa taarifa zinazodai kuwa inamtaka pia kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson.
Kocha wa Man City, Pep Guardiola, anaona Enzo ndiye kiungo sahihi wa kuvaa viatu vya Bernardo Silva atakapoondoka mwishoni mwa msimu huu.
Wakati huo huo, mkataba wa Rodri utafikia ukomo mwaka 2027, ingawa Guardiola anaamini ‘mido’ huyo raia wa Hispania ataongeza mwingine.
Enzo mwenye umri wa miaka 25, bado ana mkataba na Chelsea utakaofikia ukomo mwaka 2032.






