MILAN, Italia
MANCHESTER United na Liverpool zimeingia kwenye ushindani mkali wa kuiwania saini ya winga wa AC Milan, Rafael Leao.
Wakati huo huo, Manchester City na Real Madrid nazo zimetajwa kwenye mbio za kumsaka Mreno huyo.
Leao amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu, ambapo ameshafunga mabao katika mechi za Ligi Kuu ya Italia (Serie A).
Ripoti zinaeleza kuwa Milan watakuwa tayari kumpiga bei nyota wao huyo endapo watawekewa mezani kitita cha Pauni milioni 60.
Dau hilo linatokana na miaka miwili iliyobaki kwenye mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
Gazeti la Daily Mail limedai kuwa Leao hana maelewano mazuri na kocha wa sasa wa Milan, Max Allegri.






