WASHINGTON DC, Marekani
RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema Israel na Lebanon zimekubaliana kuongeza wiki tatu za kusitisha mapigano.
Wakati huo huo, Rais Trump ameeleza kuwa hana wasiwasi juu ya mpango wake wa kufikia makubaliano na Iran.
Amezungumzia hilo akihusianisha na hatua ya jeshi la Marekani kuizuia meli ya mafuta ya Iran katika Bara ya Hindi.
“Marekani ina udhibiti kamili wa Mlango-Bahari wa Hormuz,” amesema Rais Trump.
Kwa upande wake, Wizara ya Ulinzi ya Israel imedai kuwa iko tayari ‘kufufua’ vita yake na Iran endapo itapata ruhusa ya Marekani.
Katika hatua nyingine, jeshi la Israel limewashutumu wapiganaji wa Hezbollah kwa kuendeza mashambulizi wakati huu wa makubaliano ya kusitisha vita.






