Wazirti wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu |
 NA CHARLES MULLINDA
SERIKALI ya Awamu ya Tano imefanikiwa kuokoa asilimia 11 ya vifo vya watu wake vilivyokuwa vikisababishwa na ugonjwa wa kipindupindu.
Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Gerard Chami katika mahojiano maalumu ya Tanzania PANORAMA Blog.
Chami alisema ugonjwa wa kipindupindu ulitokomezwa rasmi hapa nchini Julai mwaka Jana na tangu wakati huo hadi sasa Tanzania haijapata mtu mwenye mgonjwa huo.
“Taarifa ya kutokomezwa kwa ugonjwa wa kipindupindu ilishatolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Leonard Subi akizindua kikao kazi cha kufanya tathimini, maboresho na kuandaa mpango kazi wa miaka mitano katika kukabiliana na ugonjwa huo hapa nchini.
“Hapa nirejee kukariri kauli ya Dk. Subi kuwa tangu Julai 2019, Tanzania hatuna Kesi yoyote ya ugonjwa wa kipindupindu.
“Kwa miaka kadhaa halo nyuma tulikuwa na takriban asikimia 11 ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa kipindupindu lakini kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika maeneo tofauti ikiwemo kuimarishwa kwa miundombinu ya kutolea huduma za afya na upatikanaji wa dawa na vifaa.
” Pia vifaa tiba na vitendanishi, kaya karibu zote nchini kuwa na vyoo safi na bora, kuimarishwa kwa usafi wa mazingira na upatikanaji wa maji safi na salama, kipindupindu kilipungua hadi kufikia asilimia 1.7 na kwa kipindi cha mwa jana hadi sasa hatuna mgonjwa akiyetolewa taarifa ya kuwa na maambukizi hayo,” alisema Chami.
Alisema kazi inayofanywa sasa na serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni kuchambua mpango kazi wa miaka mitano wa udhibiti wa ugonjwa huo, kufanya ufuatiliaji, tathmini na uperembaji wa afua mbalimbali za Afya hapa na kujua na mpango kazi wa utekezaji wa kimkakati.
Mwisho
Â