Friday, December 27, 2024
spot_img

ACT WAZALENDO CHAMKINGIA KIFUA MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD

 

Jaji Francis Mutungi

NA MWANDISHI WETU

CHAMA cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) kimemwandikia barua msajili wa vyama vya siasa, kikijibu barua yake iliyokitaka kijieleza kwa kukiuka masharti ya kifungu cha 11 A cha sheria ya vyama vya siasa.

ACT katika baru yake hiyo kimemtaka msajili arejee na kufahamu tafasiri sahihi ya kifungu hicho.

Barua hiyo ya Septemba 24, 2020 yenye kumbukumbu namba ACT/HQ/MSJ/023/Vol.III/248 inamtaka msajili afahamu maana, tafasiri sahihi na tofauti ya vyama kuungana chini ya kifungu hicho na mgombea mmoja kuonyesha imani yake kwa mgombea mwingine katika uchaguzi mkuu.

Kwa mujibu wa barua hiyo ambayo imesainiwa na Jaran Bashange kwa niaba ya katibu mkuu, mgombea mmoja kuonyesha imani kwa mgombea mwingine ni jambo la kupigiwa mfano kwa siasa za Tanzania kuwa licha ya ushindani wa kisiasa, umoja na mshikamano kama watanzania unadumishwa.

Sehemu ya barua hiyo ambayo Tanzania PANORAMA Blog imeoina inasomeka; ‘nakiri kupokea barua yako ya tarehe 22 Septemba, 2020 yenye kumbukumbu namba HA.322/362/21/90 inayotutaka tuwasilishe maelezo juu ya mgombea wetu wa urais wa Zanzibar, Mheshimiwa Seif Sharif Hamad kumuombea kura mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tundu Antipas Lissu

‘Katika barua yako umetukumbusha uwepo wa kifungu cha 11 A cha sheria ya vyama vya siasa kinachoweka utaratibu wa vyama “kushirikiana” na ukaenda mbali kuwa kwa vyama kushirikiana bila kufuata utaratibu uliowekwa ni kukiuka sheria.

‘Tunapenda kueleza kuwa mgombea wetu wa urais wa Zanzibar, mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad hajakiuka kifungu cha 11 A cha sheria ya vyama kinachoweka utaratibu wa vyama kuungana au vinavyokusudia kuungana kabla au baada ya uchaguzi.

‘Aidha, mheshimiwa Seif Sharif Hamad hakumuombea kura ndugu Tundu Antipas Lissu kama inavyodaiwa na ofisi yako. Video clip uliyotutumia haina maneno hayo na nikuombe urejee kuisikiliza upya kwa makini .

‘Alichokisema mgombea wetu ni imani yake kuwa ndugu Tundu Antipas Lissu atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jambo ambalo liko wazi sana kutokana na mwelekeo wake wa kuungwa mkono na watanzania walio wengi.

‘Hii inathibitishwa na namna wananchi wengi na kwa hamasa kubwa wanavyojitokeza katika mikutano yake ya kampeni inayoendelea. Hilo si kosa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.

Maalim Seif na Zitto Kabwe


‘Kauli na imani hiyo haina tafasiri ya kuungana kwa vyama vyetu vya Alliance for Change and Transparent (ACT Wazalendo) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ila chama chetu kina imani kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chama Cha Mapinduzi, Ndugu John Pomne Magufuli hatakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya uchaguzi wa tarehe 28 Oktoba, 2020.’

Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa ilikiandikia ACT ikikitaka kitoe maelezo kuhusu hatua ya Maalim Seif kumuombea kura mgombea urais wa Chadema, Lissu.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya