JELA MIAKA 30 KWA KUPATIKANA NA BANGI

Date:

Share post:

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya imemhukumu Brown Frank Mwaitubi (31), mkazi wa Kajunjumele, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

Hukumu hiyo imetolewa Aprili 24, 2026 na Hakimu wa Mahakama hiyo, Rosta Mofuga, baada ya mshitakiwa kukutwa na kete 20 za bangi zenye uzito wa gramu 896.35.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa Mwaitubi alitenda kosa hilo Agosti 18, 2025 baada ya askari kumkuta akiwa amehifadhi dawa hizo nyumbani kwake kwa lengo la kuziuza.

Mshitakiwa alitiwa hatiani kwa mujibu wa kifungu cha 16(1) na 16(2)(c) cha Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya, Sura ya 95, Marejeo ya mwaka 2023.

Akiwasilisha hoja zake mahakamani, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Wakili Brice Kessi (SA), aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa mtuhumiwa pamoja na jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

DUTERTE KUPANDISHWA KIZIMBANI ICC

MANILA, Ufilipino JOPO la majaji watatu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) limethibitisha kuwa Rais wa zamani wa...

WRIGHT: RICE APEWE BALLON D’OR

LONDON, Uingereza MKONGWE wa Arsenal, Ian Wright, amemtaja Declan Rice kuwa anastahili kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka...

ISRAEL, LEBANON ZAONGEZA WIKI TATU ZA KUSITISHA VITA

WASHINGTON DC, Marekani RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema Israel na Lebanon zimekubaliana kuongeza wiki tatu za kusitisha mapigano. Wakati...

RAIS RAMAPHOSA ‘AMTUMBUA’ MKUU WA POLISI

PRETORIA, Afrika Kusini RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ametengua uteuzi wa Mkuu wa Polisi nchini humo, Jenerali Fannie...