DUTERTE KUPANDISHWA KIZIMBANI ICC

Date:

Share post:

MANILA, Ufilipino

JOPO la majaji watatu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) limethibitisha kuwa Rais wa zamani wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, atapandishwa kizimbani.

Duterte anakabiliwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu, hasa kwa operesheni yake ya kupinga dawa za kulevya akiwa Rais kuanzia mwaka 2016 hadi 2022.

ICC inadai kuwa operesheni hiyo ya Duterte ilisababisha vifo vingi tangu alipoianza akiwa Meya hadi alipoingia Ikulu.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanaeleza kuwa watu 30,000 walipoteza maisha wakati wa operesheni zake hizo.

Mahakama ya ICC imeeleza kuwa ina ushahidi wa kutosha wa kuendeleza mashitaka dhidi yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

WRIGHT: RICE APEWE BALLON D’OR

LONDON, Uingereza MKONGWE wa Arsenal, Ian Wright, amemtaja Declan Rice kuwa anastahili kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka...

ISRAEL, LEBANON ZAONGEZA WIKI TATU ZA KUSITISHA VITA

WASHINGTON DC, Marekani RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema Israel na Lebanon zimekubaliana kuongeza wiki tatu za kusitisha mapigano. Wakati...

RAIS RAMAPHOSA ‘AMTUMBUA’ MKUU WA POLISI

PRETORIA, Afrika Kusini RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ametengua uteuzi wa Mkuu wa Polisi nchini humo, Jenerali Fannie...

PAPA AKOSOA MATESO YA WAFUNGWA GUINEA

MALABO, Guinea ya Ikweta KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, ameeleza kutokuridhishwa na namna wafungwa wanavyoishi katika...