LONDON, Uingereza
MKONGWE wa Arsenal, Ian Wright, amemtaja Declan Rice kuwa anastahili kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya Ballon d’Or msimu huu.
Wright amesema endapo Arsenal itatwaa mataji ya Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa, basi kiungo huyo atastahili tuzo hiyo.
Lejendari huyo ameyasema hayo katika mahojiano yake na kipindi cha televisheni ya mtandaoni ya ‘Stick to Football’.
“Kama Arsenal itakuwa bingwa wa Ligi Kuu, Declan Rice anapaswa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi,” amesema Wright.
“Na kama Arsenal itakuwa bingwa wa Ligi ya Mabingwa, basi atapaswa kuwa mshindi wa Ballon d’Or.”
Rice (27), alisajiliwa na Arsenal mwaka 2023 akitokea kwa majirani zao wa London, West Ham United, ambapo dili hilo liligharimu Pauni milioni 105.






