Friday, December 27, 2024
spot_img

‘VITAMBULISHO VYA MACHINGA VIMETUTUAMZIGO’

 

NA PIUS NTIGA, MOSHI

WAFANYABIASHARA wadogo, maarufu kwa jina la Machinga katika Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamesema vitambulisho wa wajasiriamali wadogo vimewatua mzigo hivyo wanawashangaa baadhi ya wanasiasa wanaopotosha kuhusu vitambulisho hivyo.

Wakizungumza na Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM inayoangazia mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, wafanyabiashara hao wamesema utamu wa vitambulisho hivyo wanaujua wao.

Wamesema awali walikuwa wanalipa shilingi 500 kwa siku, sawa na shilingi 182,000 kwa mwaka, kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha na shilingi 20,000 wanayolipa sasa kwa mwaka.


“Tulikua tukilipa shilingi 200 ya usafi kwa siku, sawa na shilingi 73,000 kwa mwaka, ambapo sasa mateso kama hayo hatuyapati. Tena tunashukuru sana Rais Magufuli kwa kutuona na tutampa zawadi mwaka huu” wamesema Machinga.

Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao wadogo, mkombozi wao ni Rais Magufuli ambaye amekuja na mpango wa sh 20,000 tu kwa mwaka na sasa kero za mgambo kuwafukuza hazipo tena.


“Nikwambie tu kuwa mabenki nayo yamesema kwa kuwa tuna vitambulisho, shughuli zetu zimerasimishwa hivyo tumeanza kupewa mikopo huku vitambulisho vikiwa ni dhamana yetu,” wamesema

Wamesema hivi sasa hawasumbuliwi tena na askari wa jiji wala mgambo kama ilivyokuwa hapo awali.

“Vitambulisho vya wamachinga vimetusaidia sana, tunanunua kwa ridhaa yetu, hatulazimishwi,” wamesema Machinga.

Aidha, wamefafanua kuwa uwepo wa vitambulisho hivyo umewaondolea kero na kwa sasa biashara yao imeimarika zaidi na kipato chao kimeongezeka na wamefanikiwa kununua ardhi na kujenga nyumba.


Kutokana na mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Moshi, Michael Mwandezi, amesema tangu kuanza kwa utaratibu huo zaidi ya asilimia 70 ya wamachinga wamepatiwa vitambulisho katika Manispaa ya Moshi.

Mwandezi amesema fedha inayotokana na vitambulisho hivyo inakwenda Hazina na kisha kurudishwa katika Manispaa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo inawagusa moja kwa moja wananchi.

“Pia tumewasaidia hawa wajasiriamali kuwajengea uwezo wa kimtaji ambapo sasa wanakopesheka kupitia vitambulisho, hivyo vimewanufaisha kwa kukopa fedha benki,” amesema Mkurugenzi huyo

Hivi karibuni baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipotosha kuhusu vitambulisho vya wamachinga kuwa haviwanufaishi na badala yake wanaibiwa, kauli ambayo Rais John Magufuli ambaye ni mgombea wa urais kupitia CCM, amewataka wafanyabiashara hao kuwapuuza wanasiasa hao na badala yake waunge juhudi za serikali za kuwakomboa wamachinga. 

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya