MAKACHERO WANAOCHUNGUZA KASHFA YA UNYANYASAJI KINGONO WALALAMIKIWA

Date:

Share post:

 

NA MWANDISHI WETU

MLALAMIKA katika shauri la madai ya kunyanyaswa kingono (jina limehifadhiwa) amewaelekezea lawama makachero wa polisi wa Kituo cha Chang’ombe wanaochunguza shauri lake kuwa wameuweka pembeni ushahidi muhimu wa madai yake.

Amesema makachero hao ambao wameizuia simu yake ya mkononi kwa uchunguzi hawakuchukua simu ya anayemtuhumu ambayo ina ushahidi muhimu wa kuthibitisha madai yake.

Mlalamikaji huyo anamtuhumu Dreva wa Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB), anayefahamika kwa jina la Idi Mzee kumnyanyasa kingono.

Kamanda wa Upelelezi (RCO) wa Kituo cha Polisi Chang’ombe, Jumanne Mkwama amekwishathibitisha kuwepo kwa shauri hilo kwa kueleza kuwa simu za mlalamikaji na mlalamikiwa zimepelekwa kwa watalaamu kuchunguzwa.

Kamanda Mkwama aliieleza Tanzania PANORAMA Blog kuwa kinachochunguzwa na makachero wake ni nani kati ya wawali hao aliyevunja mkataba wa kuachana lakini madai mengine yataamriwa mahakamani.

“Sina imani na wapelelezi wa shauri langu. Mimi na Idi katika mambo yetu ya hovyo tulikuwa tunawasiliana kwa WhatsApp. Na hiyo laini yake yenye WhatsApp ndiyo alikuwa akinitumi hela nyingi.

“Ajabu walichukua simu yangu ya WhatsApp lakini ya kwake wakamuachia wakachukua ya kitochi ambayo haina ushahidi wa maana. Niliwaambia simu yake ya WhatsApp ndiyo ina mambo yetu yote wakasema hiyo hawaitaki wanataka kile kitochi.  Nina wasiwasi wanataka kuficha kitu au kumlinda,” alisema.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

EMERY APANGA KUIBOMOA BARCELONA

LONDON, Uingereza KOCHA wa Aston Villa, Unai Emery, anaitaka saini ya beki wa Barcelona, Alejandro Balde, na amewaambia mabosi...

BAYERN YAMKODOLEA MACHO KIUNGO WA TOTTENHAM

LONDON, Uingereza BAYERN Munich inampigia hesabu za karibu kiungo wa Tottenham na timu ya Taifa ya Senegal, Pape Matar...

RIPOTI: IDADI YA WAHAMIAJI ULAYA IMEVUNJA REKODI, UJERUMANI INAONGOZA

LONDON, UingerezaRIPOTI mpya imeonesha kuwa Ulaya nchi za Ulaya zlipokea wahamiaji milioni 64 mwaka 2025, likiwa ni ongezeko...

RAIS WA TAIWAN ASITISHA ZIARA YAKE AFRIKA, CHINA IKITAJWA KUWA CHANZO

TAIPEI, TaiwanRAIS wa Taiwan, Lai Ching-te, ameahirisha ziara yake nchini Eswatini, huku akiitaja China kuwa ndiyo chanzo cha...