WANASHERIA WACHAMBUA KESI INAYOMUHUSU DREVA WA SSB

Date:

Share post:

 

NA MWANDISHI WETU

KITENDO cha kumshawishi mtu kufanya mapenzi na mnyama au watu wawili kufanya mapenzi mbele ya mtu mwingine au mbele ya kadamnasi ya watu ni kosa jinai.

Hayo yameelezwa na wanasheria waliozungumza na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu sakata linalomuandama Idi Mzee ambaye ni dreva wa Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) anayelalamikiwa na mpenzi wake, jina limehifadhiwa kuwa amekuwa akimfanyisha mapenzi na mbwa, kumfanyisha mapenzi na wanawake wenzake, kumfanyisha mapenzi na wanaume zaidi ya mmoja huku yeye akiwaangalia kabla ya kushiriki naye tendo hilo na pia kumfanyisha mapenzi kinyime cha maumbile.

Hata hivyo, wanasheria hao waliozungumza kwa sharti la majina yao kuhifadhiwa kwa kile walichodai kuwa madai hayo yanatia kinyaa, wamesema mwanasheria anayedaiwa kusimamia mkataba wa wapenzi hao kuachana kwa sharti la kulipana pesa hana hatia na alichokifanya hamkimfungi kisheria.

“Mwanasheria anayedaiwa kusimamia mkataba wa wapenzi hao kuachana, na sitaki kumtaja jina mimi hata kama ametajwa kwa sababu ya jambo lenyenye hili lilivyo hana kosa lolote. Hata kama alijua matendo machafu ya watu hao hana kosa. Mwanasheria ni kama karani tu.

“Na huo mkataba aliowasainisha na kulipana fedha kama inavyodaiwa, pamoja na kwamba aliuandaa yeye kama inavyodaiwa lakini hautambuki kisheria.

“Lakini sasa, kitendo cha kufanya mapenzi na mbwa ni kosa kisheria na mtu yoyote anayemshawishi mtu mwingine kufanya mapenzi na mbwa anakuwa ametenda kosa la jinai. Hilo haliko katika makosa ya madai,” alisema mmoja  wa wanasheria waliozungumza na Tanzania PANAROMA Blog.

Mwanasheria mwingine aliyezungumzia hilo alisema binadamu kufanya mapenzi na wanyama hairuhusiwi kisheria.

“Binadamu kufanya mapenzi na mnyama hairuhusiwi kisheria na au kufanya mapenzi kinyume cha maumbile au kufanya mapenzi na mtu zaidi ya mmoja.

“Sisi kama taifa la watu wastaarabu tena wenye utamaduni mzuri kabisa tunapaswa kuyapiga vita kwa nguvu zetu zote mambo ya aina hii pasipo kuagaliana usoni.

“Mwaka 2008, huko mkoani Mwanza, Hakimu  Gadiel Mariki aliwahukumu watu watatu kwenda jela miaka 20 kwa makosa ya kushawishi na kufanya mapenzi na mbwa. Hawa walikuwa wafanyakazi wa kampuni moja inayojihusisha na uchumbaji madini hapa nchini hivyo ni lazima watu waelewe kufanya mapenzi na wanyama au mbele ya mtu mwingine ni makosa makubwa kisheria,” alisema.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

EMERY APANGA KUIBOMOA BARCELONA

LONDON, Uingereza KOCHA wa Aston Villa, Unai Emery, anaitaka saini ya beki wa Barcelona, Alejandro Balde, na amewaambia mabosi...

BAYERN YAMKODOLEA MACHO KIUNGO WA TOTTENHAM

LONDON, Uingereza BAYERN Munich inampigia hesabu za karibu kiungo wa Tottenham na timu ya Taifa ya Senegal, Pape Matar...

RIPOTI: IDADI YA WAHAMIAJI ULAYA IMEVUNJA REKODI, UJERUMANI INAONGOZA

LONDON, UingerezaRIPOTI mpya imeonesha kuwa Ulaya nchi za Ulaya zlipokea wahamiaji milioni 64 mwaka 2025, likiwa ni ongezeko...

RAIS WA TAIWAN ASITISHA ZIARA YAKE AFRIKA, CHINA IKITAJWA KUWA CHANZO

TAIPEI, TaiwanRAIS wa Taiwan, Lai Ching-te, ameahirisha ziara yake nchini Eswatini, huku akiitaja China kuwa ndiyo chanzo cha...