LONDON, Uingereza
BAYERN Munich inampigia hesabu za karibu kiungo wa Tottenham na timu ya Taifa ya Senegal, Pape Matar Sarr.
Tottenham ilimsajili Sarr mwaka 2021, kisha ikampeleka kwa mkopo Mainz, kabla ya kumrudisha na kuwa mchezaji tegemeo tangu mwaka 2023.
Kwa miaka mitatu, nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 ameshacheza mechi 135 na kufunga mabao 11.
Kwa mujibu wa mtandao wa Football Insider, Bayern, Fenerbahce na Real Madrid zinapigana vikumbo kuinasa saini yake.
Kwa sasa, bado mchezaji huyo ana mkataba na Tottenham, ambao unatarajiwa kufikia ukomo mwaka 2030.






