IRAN: TUKO TAYARI KWA VITA MAZUNGUMZO YAKISHINDIKANA

Date:

Share post:

TEHRAN, Iran
SPIKA wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema nchi yake itakuwa tayari kwa mbinu mpya za kivita endapo utakosekana mwafaka katika mazungumzo ya amani na Marekani.

Kesho Aprili 22, 2026 ndiyo siku ya mwisho ya kile kilichokubaliwa kuwa ni wiki mbili za kusitisha mapigano.

Pande mbili hizo zilikubaliana kusitisha vita ili walau kutoa nafasi ya mazungumzo ya kusaka suluhu katika mgogoro huo unaofukuta Mashariki ya Kati.

Hata hivyo, mazungumzo yaliyofanyika siku chache mjini Islamabad, Pakistan, hayakuzaa matunda, huku kila upande ukiushutumu mwingine kwa kuweka misimamo mikali.

Kwa sasa, zipo jitihada za kufanikisha mazungumzo mengine, ingawa bado kumekuwa na mvutano unaotishia uwezekano wa kutokufanyika.

Viongozi wa Iran wamesema mara kadhaa kuwa hawatoshiriki kwa kuwa Marekani haina nia ya dhati ya kupata maridhiano kutokana na aina ya masharti inayotoa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RAIS WA TAIWAN ASITISHA ZIARA YAKE AFRIKA, CHINA IKITAJWA KUWA CHANZO

TAIPEI, TaiwanRAIS wa Taiwan, Lai Ching-te, ameahirisha ziara yake nchini Eswatini, huku akiitaja China kuwa ndiyo chanzo cha...

USIYOYAJUA KUHUSU ZIARA YA PAPA LEO BARANI AFRIKA

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, yuko barani Afrika kwa ziara ya siku 10 katika mataifa...

MATESO WANAYOPITIA WATOTO KATIKA MACHAFUKO YA SUDAN

DARFUR, Sudan "HALI ya watoto nchini Sudan inazidi kuwa mbaya kila baada ya saa moja." Hiyo ni kauli ya...

RAIS WA BRAZIL AMVAA TRUMP, AITAKA AFRIKA KUSINI KUMPUUZA

BERLIN, Ujerumani RAIS wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, amesema Donald Trump hana mamlaka ya kumzuia Cyril Ramaphosa...