SANAMU YA YESU YAMPONZA MWANAJESHI WA ISRAEL

Date:

Share post:

BEIRUT, Lebanon

MWANAJESHI wa Israel aliyeonekana akiharibu sanamu ya Yesu wakati wa operesheni yao nchini Lebanon ameanza kuchunguzwa.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amelaani kitendo kilichofanywa na mwanajeshi huyo, akisema ameshangazwa na kusikitishwa.

Katika picha zilizosambaa mitandaoni, ambazo Israel imekiri kuwa siyo za kutengeneza, mwanajeshi huyo ameonekana akipiga kichwa cha sanamu hilo kwa nyundo.

Israel haikuweka wazi eneo la tukio, ingawa inafahamika kuwa wanajeshi wake wana udhibiti mkubwa maeneo ya Kusini mwa Lebanon.

Aidha, Netanyahu amesema tayari mamlaka za Israel zimeanza uchunguzi juu ya tukio hilo ili kumchukulia hatua mwanajeshi huyo.

Kama hiyo haitoshi, jeshi la Israel limewaahidi wakazi wa eneo hilo kuwa litagharamia ukarabati wa sanamu lao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RAIS WA TAIWAN ASITISHA ZIARA YAKE AFRIKA, CHINA IKITAJWA KUWA CHANZO

TAIPEI, TaiwanRAIS wa Taiwan, Lai Ching-te, ameahirisha ziara yake nchini Eswatini, huku akiitaja China kuwa ndiyo chanzo cha...

USIYOYAJUA KUHUSU ZIARA YA PAPA LEO BARANI AFRIKA

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, yuko barani Afrika kwa ziara ya siku 10 katika mataifa...

MATESO WANAYOPITIA WATOTO KATIKA MACHAFUKO YA SUDAN

DARFUR, Sudan "HALI ya watoto nchini Sudan inazidi kuwa mbaya kila baada ya saa moja." Hiyo ni kauli ya...

IRAN: TUKO TAYARI KWA VITA MAZUNGUMZO YAKISHINDIKANA

TEHRAN, IranSPIKA wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema nchi yake itakuwa tayari kwa mbinu mpya za...