Wednesday, 7 October 2026

SIKIA HII! DAVIDO, CHRIS BROWN WANA JAMBO LAO

LAGOS, Nigeria SUPASTAA wa Afrobeats, Davido, amewaweka mkao wa kula mashabiki wake, akisema wajiandaye kwa ‘kolabo’ yake na mkali wa R&B nchini Marekani, Chris Brown. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Davido amedai kuwa mzigo huo utaingia sokoni mapema mwakani. Hata hivyo, amesema kwa sasa ngoma zake zitajikita katika vionjo vya Kiafrika, licha ya kwamba […]

LAGOS, Nigeria

SUPASTAA wa Afrobeats, Davido, amewaweka mkao wa kula mashabiki wake, akisema wajiandaye kwa ‘kolabo’ yake na mkali wa R&B nchini Marekani, Chris Brown.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Davido amedai kuwa mzigo huo utaingia sokoni mapema mwakani.

Hata hivyo, amesema kwa sasa ngoma zake zitajikita katika vionjo vya Kiafrika, licha ya kwamba atakuwa akiwashirikisha mastaa wa kimataifa.

“Muziki ninaotengeneza kwa sasa ni wa Kiafrika. Hata katika ngoma zangu zijazo, nitafanya na maprodyuza wangu wa zamani,” amesema.

Davido na Chris Brown walianza kushirikiana katika ngoma mwaka 2019. Kolabo yao ya kwanza iliyofanya vizuri ni ‘Blow My Mind’. Wawili hao wana nyimbo tano walizofanya pamoja.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *