HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha ‘Ma-dj’ nchini Nigeria, ambao walipiga marufuku nyimbo zake kuchezwa.

Chama hicho kiliwataka wanachama wake kutokutumia ngoma za Burna Boy, iwe kwenye vipindi vya redio, runinga, matamasha au sherehe.

Chanzo ni staa huyo na watu wake kumpiga Dj Tunez katika moja ya matamasha, ikielezwa kuwa walikerwa na kitendo chake cha kucheza nyimbo za Wizkid.

Kwa upande mwingine, hii si mara ya kwanza kwa Burna Boy kuingia kwenye shida na mastaa wenzake. Kuna orodha ndefu ya watu maarufu aliowahi kutibuana nao.

DAVIDO

Ni bifu lililoanzia mwaka 2009 lakini lilikolea zaidi mwaka 2020 baada ya wawili hao kuripotiwa kurushiana makonde wakiwa nchini Ghana.

Inaelezwa kuwa wawili hao walikutana katika klabu moja ya starehe nyakati za usiku na siku hiyo Wizkid naye alikuwepo lakini hakujishughulisha na ugomvi wao.

WIZKID

Burna Boy na Wizkid waliwahi kuwa marafiki wakubwa. Ugomvi wao ulisababishwa na shabiki huko mitandaoni. Ilikuwaje?

Shabiki alisema Wizkid ndiye anayefanya vizuri zaidi sokoni. Kauli hiyo ilimkera Burna Boy na kusema kama si urafiki, angempiga Wizkid.

Kuanzia hapo, Burna Boy na Wizkid wakawa ‘chui na paka’, ikawa ni nadra na baadaya haiwezekani kabisa kuwaona wawili hao wakiwa pamoja kama zamani.

AKA

Waliwahi kuwa marafiki pia, wakishirikiana katika nyimbo kadhaa zilizofanya vizuri Nigeria na hata Afrika Kusini anatokea AKA.

Bifu lilianzia wakati wa sekeseke la raia wa Afrika Kusini kuwashambulia wahamiaji wanaoingia nchini humo, kwa madai kuwa wanapunguza ajira na kufanya maisha uawe magumu.

AKA alitoa kauli za aina hiyo pia, jambo ambalo Burna Boy hakufirahishwa nalo. Vita yao ikaanzia hapo, mwaka 2019.

SPEED DARLINGTON

Uhusiano wao mbaya ulianzia pale Speed Darlington aliposema P. Diddy alikuwa na mchango wakati Burna Boy aliposhinda tuzo ya Grammy.

Kama itakumbukwa, kauli hiyo ilimchefua Burna Boy na hatua yake ya kwanza ikawa ni kumshitaki rapa huyo, kisha polisi wakamkamata, ingawa aliachiwa baadaye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here