WAZAZI WA MWANAFUNZI ALIYEPOTEA ST MARY’S WADAI KUPEWA SIRI NYETI NA MKUU WA SHULE

Date:

Share post:

 

NA MWANDISHI WETU

WAZAZI wa mwanafunzi aliyepotea tangu Oktoba 4, 2020 Labna Salim Said wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Bweni Wasichana ya St Mary’s iliyopo Mbezi Makonde, Dar es Salaam wamesema Mkuu wa Shule hiyo, Reca Ntipoo aliwafichulia siri nyeti inayowawezesha wanafunzi kutoroka usiku kwenda kufanya ukahaba.

Mwanafunzi Labna anadaiwa kutoroka shuleni usiku akiwa na wenzake na kwenda kwa wanaume lakini tofauti na wenzake ambao walirejea shuleni kabla ya kupambazuka, yeye hakurejea na haifahamiki yupo wapi hadi sasa.

Taarifa za kutoweka kwake ziliripotiwa kwa mara yake na matroni anayetajwa kwa jina Sarah Murra lakini katika hatua ya kushangaza, uongozi wa Shule ya St Mary’s haujapata kuripoti tukio hilo polisi na sasa wazazi wa mwanafunzi huyo wanahofia kuwa ameuawa.

“Mkuu wa Shule alituambia kuwa ukuta wa shule hiyo ni mfupi unaowawezesha wanafunzi kuruka kwa urahisi na alisema shule ina walinzi wachache ambao hawatoshelezi kulinda eneo lote la shule ndiyo maana ni rahisi kwa wanafunzi kutoroka usiku,” alisema Maduhu.

Mkuu wa shule hiyo, Ntipoo kwa siku kadhaa sasa simu yake imekuwa ikiita bila kupokewa .

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

RAIS WA UTURUKI AIONYA ULAYA KUHUSU IRAN

ISTANBUL, Uturuki RAIS wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema vita kati ya Iran na Marekani vimeanza kulidhohofisha Bara la...

ISRAEL YASHUTUMIWA MAUAJI YA MWANDISHI LEBANON

BEIRUT, Lebanon LEBANON imeishutumu Israel ikiihusisha na kifo cha mwandishi wa habari aliyeuawa katika shambulizi la anga. Amal Khalil aliuawa...

TRENI ZAGONGANA NA KUJERUHI ABIRIA 10 DENMARK

COPENHAGEN, DenmarkAJALI ya treni mbili za abiria zilizogongana imesababisha watu wanaotajwa kufikia 10 kujeruhiwa nchini Denmark. Kwa mujibu wa...

MABORESHO YA MKOA WA KATAVI KUWEKWA KWENYE GRIDI YA TAIFA YA UMEME YA KAMILIKA

Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Serikali imekamilisha kuunganisha Mkoa wa Katavi katika Gridi ya Taifa na hivyo...