KISWAHILI CHAKWAMISHA KESI MAHAKAKANI

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA, ARUSHA

MAHAKAMA ya Afrika Mashariki (EACJ) leo imeshindwa kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Baraza la Serikali ya Kijiji cha Ololosokwan kwa sababu hati ya mashitaka imeandaliwa kwa Lugha ya Kiswahili.

Baraza la Serikali ya Kijiji cha Ololosokwan kilicho Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha limefungua kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania likiiomba EACJ iizuie Serikali kuwahamisha wanakijiji wa Kijiji hicho kwenye ardhi wanayoishi.

Shauri hilo liko mbele ya majaji watatu wa EACJ wakiongozwa na Jaji Kiongozi, Monica Mugenyi ambaye aliahirisha shauri hilo kwa maelezo kuwa hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani, kwenye kesi namba 15 ya mwaka 2017 ina kasoro kwa sababu imeandikwa kwa Lugha ya Kiswahili badala ya Lugha ya Kiingereza ambacho kinatambulika mahakamani hapo.

Aidha, alisema hati zimesainiwa na mawakili wawili tofauti hivyo mahakama imeshindwa kujua itumie hati gani ya mashtaka.

“Hati hizi zimesainiwa na mawaikili wawili tofauti, hakuna hati ya kiapo inayoonyesha ni halali na imefuata taratibu za kimahakama. Lakini pia mmeandika kwa Lugha ya Kiswahili wakati mnajua mahakama hii inatumia Lugha ya Kingereza.

“Kutokana na kasoro hizo tunalazimika kuahirisha kesi hii hadi hapo mtakaporekebisha kasoro mbalimbali zilizopo kwenye hati ya kiapo,” alisema Jaji Mugenyi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...