MJUKUU APANGA MAUAJI YA BABU YAKE KWA MILIONI MOJA

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA, RUKWA

MZEE mwenye umri wa miaka 72 aliyefahamika kwa jina la Paul Kisiwa, mkazi wa Kijiji cha Ng’ongo ameuawa kwa kupigwa rungu kichwani.

Mzee huyo aliuawa Machi 3, mwaka huu majira ya jioni katika Kijiji cha Kifinga kilicho Kata ya Mtowisa wilayani Sumbawanga.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando ambaye amesema watu sita akiwemo mjukuu wa mzee huyo wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kupanga mauaji hayo.

Kamanda Kyando alisema mjukuu wa mzee Kisiwa ambaye hakumtaja jina alikubali kuchukua Sh. Milioni moja ili babu yake auawe.

Diwani wa Kata ya Mtowisa, Edger Malinyi naye amekaririwa akieleza kuwa mzee huyo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alizikwa kimya kimya shambani kwake baada ya kuuawa.

“Taarifa za kupotea kwa Kisiwa zilianza kuzagaa. Ndugu na jirani zake wakishirikiana na polisi walianza kumtafuta ilipofika Machi 8, mwaka huu walimbana mjukuu wake ambaye alikiri kupanga njama za kumuua babu yake baada ya kupewa Sh. 1,000,000. Alipobanwa alieleza kuwa alipanga njama za mauaji hayo na watu waliokuwa na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu na babu yake.

“Kwamba babu yake aliwakodishia watu hao shamba la ekari zaidi 15 kwa ajili ya shughuli za kilimo lakini baadaye aliwanyang’anya akaanza kulilima mwenyewe ndiyo wakakasirika wakaandaa mpango wa kumuua.

“Siku ya tukio la mauaji walimvamia akiwa shambani kwake, wakampiga na rungu kichwani ambalo lilimuua papo hapo.

“Baada ya kumuua, walichimba shimo shambani humo wakamzika ili kupoteza ushahidi. Mjukuu wake alionyesha mahali alipozikwa na polisi walipofukua waliukuta mwili wa mzee huyo,” alisema diwani huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...