LONDON, Uingereza
KLABU ya Newcastle United itampiga bei straika raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Yoane Wissa, ambaye alisajiliwa kwa ada kubwa ya Pauni milioni 50 akitokea Brentford.
Newcastle walilazimika kufanya usajili huo wa haraka ili kuziba pengo la Alexander Isak aliyekuwa amejiunga na Liverpool.
Hata hivyo, ukiwa ni msimu wake wa kwanza klabuni hapo, Wissa hajaweza kuwa na makali aliyotoka nayo Brentford na sasa mabosi wa Newcastle wanataka kumuuza.
Hata hivyo, kwa kiwango alichonacho sasa, Newcastle inatarajiwa kupata si zaidi ya Pauni milioni 20 endapo itampiga bei mwishoni mwa msimu huu.
Wissa amefunga mabao matatu pekee msimu huu, likiwamo moja la Ligi Kuu ya England na ni chaguo la nne kwa kocha Eddie Howe.
Imeandaliwa na Hassan Mwasha






